Swahili

Download this information (PDF File, 358.3 KB)

Unaweza kutafsiri maelezo yoyote kwenye tovuti yetu kwa kutumia zana ya ReachDeck.

Bofya kwenye ikoni ya ReachDeck (mduara wa rangi ya chungwa na ishara ya spika, ambayo kawaida hupatikana kwenye kona ya juu kulia ya skrini yako).

Wakati upau wa zana wa ReachDeck unaonekana, bonyeza kwenye ikoni iliyo na mistatili miwili (ya nne kutoka kushoto).

Chagua lugha yako kutoka kwenye menyu kunjuzi.

Jua haki zako:

Mwongozo wako wa sheria za Queensland za kupinga ubaguzi na haki za binadamu

Nchini Queensland, haki zako zinalindwa na Sheria ya Kupambana na Ubaguzi ya 1991, ambayo inakataza ubaguzi, unyanyasaji wa kingono na kudhalilisha, na Sheria ya Haki za Kibinadamu ya 2019, ambayo inalinda haki 23 kwa kila mtu katika Queensland.

Sheria za haki za binadamu za Queensland zinalinda haki za kila mtu kwa:

Sheria ya Haki za Kibinadamu ina maana kwamba Bunge la Queensland linapaswa kuzingatia haki hizi linapotunga au kubadilisha sheria, na kwamba mashirika ya umma yanahitaji kutenda kwa upatanifu na haki hizi wakati yanapotenda au kufanya maamuzi.

Mashirika ya umma hutoa huduma ndani na kwa ajili ya Queensland.

Mashirika ya umma ni pamoja na idara za serikali ya jimbo, Mawaziri, shule za umma, hospitali za umma, Huduma ya Polisi ya Queensland, mabaraza ya mitaa na madiwani, na watumishi wa umma.

Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hutoa huduma za umma kwa niaba ya serikali pia huchukuliwa kuwa mashirika ya umma - kwa mfano, shirika lisilo la faida linalotoa huduma ya makazi ya umma.

Haki zinazolindwa na Sheria ya Haki za Kibinadamu si kamilifu, ambayo ina maana kwamba zinaweza kuwa chini ya vikwazo vinavyofaa.

Sheria ya Queensland ya kupinga ubaguzi inamaanisha kuwa huwezi kubaguliwa kwa sababu ya:

wakati ukiwa:

Sheria ya Kupinga Ubaguzi pia inakataza unyanyasaji wa kijinsia, na kutukana kwa misingi ya rangi, dini, jinsia, sifa za jinsia au utambulisho wa kijinsia.

Unyanyasaji wa kijinsia ni kinyume cha sheria popote unapotokea. Unyanyasaji wa kijinsia ni mwenendo wowote usiokubalika wa asili ya ngono. Inajumuisha ukaribu wa kimwili ambao haujakubali kama vile kugusana kwa njia ya ngono, mapendekezo ya ngono ambayo hayakualikwa, na maneno yenye maana ya ngono.

Udhalilishaji ni kitendo cha hadharani kinachochochea chuki dhidi ya, dharau au kejeli kali za mtu au kikundi cha watu kwa sababu ya rangi, dini, jinsia au utambulisho wa kijinsia. Ambapo hii inajumuisha tishio la unyanyasaji wa kimwili, ni kosa la jinai.

Wasiiana nasi

Ikiwa umebaguliwa, au umenyanyaswa kingono au kudhalilishwa hadharani, au ikiwa shirika la umma limezuia haki zako bila sababu, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Queensland.

Taarifa kuhusu sheria na jinsi ya kufanya malalamiko ya ubaguzi au haki za binadamu zinapatikana kwenye tovuti yetu kwa www.qhrc.qld.gov.au.

Iwapo umekumbana na unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi au ubaguzi, unaweza pia kuchagua kuripoti kwetu badala ya kutoa malalamiko rasmi, kwenye www.qhrc.qld.gov.au.

Unaweza kupigia Tume kutoka mahali popote katika Queensland bila malipo kwa 1300 130 670, Jumatatu hadi Ijumaa.

Ikiwa ungependelea kuzungumza nasi katika lugha nyingine kando na Kiingereza, unaweza kufanya hivyo kwa kuwasiliana na Translationz kwa nambari 07 4863 4444 ili kupata huduma yao unapohitaji.

Back to top